Monday, 10 August 2015

MSINGI MKUU WA HUDUMA NI UPENDO na Mchg Lazaro Emanuel




MSINGI MKUU WA HUDUMA NI UPENDO
1.   Ili huduma zetu ziweze kupanuka na kukua ni lazima upendo wa kimungu utawale na kudumu katika maisha yetu, pasipo upendo hata kama utakuwa na huduma kubwa kiasi gani, lazima utashuka tu na kupoa. 1 Kor 13:1-8
Mungu alitumia upendo kwa kutukomboa kwa njia ya upendo, ilibidi atoe kitu cha gharama kubwa (Yesu mwanae)
i.    Huo ulikuwa upendo wa gharama, upendo lazima uambatane na gharama kubwa, upate hasara kwa mambo Fulani. Yh 3:16
ii.   HUduma nyingi zimekufa kwa sababu ya kukosa mbolea inayoitwa upendo
iii.  Malumbano, masengenyo, wivu na mafarakano katika huduma kwa sababu ya kukosa upendo ambao ni tunda la Mungu

2.   Mungu aliweka Roho ya upendo ndani ya Mwanawe (Yesu Kristo).  Hivyo huduma ya Yesu Kristo imejaa upendo siku zote.
Yesu aliwapenda hata maadui zake na kuwaombea. Sidhani kama unaweza kumwombea mtu unayemchukia n aunayemsema vibaya na kutukana kwa maneno mengi.
i.    Yesu aliwapenda na kuwahurumia watu walioonewa na shetani, ndio maana huduma yake, ilikuwa na nguvu siku zote, kwa sababu alitangaza UPENDO.
ii.   YESU aliona katika ulimwengu war oho chuki ni uuaji, ndio maana alisema watendeeni mema wanaowaudhi na kuwanenea mabaya siku zote
iii.  Yohana anasema katika nyaraka, anayemchukia mwenzake ni muuaji na asiseme anampenda Mungu, atawezaje kusema anampenda Mungu wakati anamchukia mwanadamu anayemuona kwa macho, je, Mungu asiyemuona atawezaje kumpenda? Yh 2:9-11.
3.   Upendo huunganisha karama na huduma kuwa na nguvu, usione Mungu kakunyima huduma, au karama. Maana ungemuona mwenzako sii kitu kwa kuwa kiburi na chuki kwa wengine
4.   Mungu anataka kupanda huduma ya upendo kwako, unasemaje kwa maana chuki imefanya upokee matatizi, ugonjwa, huzuni, balaa, kugombana, vyeo vya duniani, kuuana kama Kaini alivyomuua ndugu yake. Hata watumishi wa Mungu wengi wamekufa kiroho na kimwili, pia kwa sababu ya kukosa upendo wa kimungu ndani yao, wanagombania fedha madaraka nk
5.   Kuanzia leo ishi katika upendo kwa huduma uliyo nayo hata kama unadharauliwa. Acha chuki utaona mkono wa Mungu ukikuinua na kukubariki. Amua kukataa roho mbaya ya chuki, maana chuki ni uzao wa shetani.  Na watumishi wake wa uzao wa Mungu, ni upendo, amani, furaha, utu wema, fadhila,  na uaminifu.
Nakemea roho ya chuki kuanzia sasa, ichukie katika jina la Yesu aliye hai Amina.

Ni mimi Rev Razaro emanuel Mpinga,
PO Box 103, Mbulu, Manyara, Tanzania, Afrika Mashariki.



No comments:

Post a Comment