Monday, 10 August 2015

KUJUA YAKUPASAYO KUTENDA – MDO 10:6 na Mchg Lazaro E. Mpinga




KUJUA YAKUPASAYO KUTENDA – MDO 10:6

Mungu alivyokuumba hajakuumba akuache vilevile tu. Kwa mambo aliyoyaumba na kuyaweka kabla hujatoka tumboni mwa mama yako, ameandaa na ameweka tayari mambo yakupasayo kuyatenda katika maisha yako.

  1. Unaweza ukajiuliza mambo gani hayo?

Kumbuka Kornelio alikuwa mwanadamu kama wewe, ulivyo mwanadamu, alikuwa na maswali kama wewe ulivyo na maswali mengi kama wayahudi, lakini aliambiwa kuwa na afanye mambo yampasayo kuyatenda.

Kornelio alikuwa sio mpagani kama unavyofikiria, alikuwa ni mtu wa dini kama wewe ulivyo na dini. Sadaka itakutolea dhambi zako na kukupokea na jehanamu. Na yeye aliwaza hay ohayo, ndio maana alitoa sadaka nyingi kuliko hata zako. Lakini kuna mambo ambayo alikuwa nayo, yasiyompendeza Mungu.

  1. Mungu ameandaa matendo mema kwa ajili yako, sii kwa wanyama na viumbe vingine
  2. Mungu ameweka wokovu sii kwa ajili ya kitu kingine, ni wewe na mimi mwanadamu
  3. Mungu ameweka mema, baraka, uzima na furaha kwa ajili yetu wanadamu

  1. Kusudi la Mungu sii kuishi katika dhambi, tabia ulizozizoea sio za Mungu.         
Baba yako ameziiga kwa baba wa kambo ambaye ni shetani Mdo 16:31

Uongo, uzinzi, ulevi, bangi, madawa ya kulevya, uchawi, tama mbaya, uwizi, ujambazi, kwenda kwa waganga wa kienyeji, uasherati nk. Sio hayo yakupasayo kuyatenda mbele za Mungu, ingawa una dini sawa kama Kornelio. Rumi 10:9

                    i.            Kuanzia leo chukua hatua ya kuacha, Mungu anakupenda Galatia 5:16-22
                  ii.            Ukiamua kuokoka kwa akili zako, huwezi kujiokoa hata kama umesoma sana. Jehanamu haikuogopi, itakumeza.
                iii.            Acha ubishi chukua Roho ya Mungu ya utii, utakula mema ya nchi mpendwa. Rumi 6:23
                iv.            Dhambi imeleta magonjwa, mauti, laana, chuki nk

Mungu akubariki. Ni mimi Rev Razaro Emanuel Mpinga


No comments:

Post a Comment